Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC) anatangaza nafasi za kujiunga na kozi za Mafunzo ya Ualimu wa Ufundi katika chuo hicho kwa mwaka wa mafunzo unaoanza Machi 2021.

1 KOZI ZA MAFUNZO

1.1 Cheti cha Ualimu wa Ufundi Stadi kwa Walimu Wasaidizi (Assistant Vocational Teacher Certificate)

Muda: Mwaka mmoja.

Sifa za kujiunga: Cheti cha Elimu ya Sekondari – Kidato cha Nne kwa ufaulu wa angalau alama ‘D’ mbili (2) bila kuhusisha masomo ya dini na Cheti cha VETA cha Ufundi Stadi Hatua ya Tatu (National Vocational Award – Level Three) katika fani yoyote.

1.2 Cheti cha Ualimu wa Ufundi na Ufundi Stadi (Technician Certificate in Technical and Vocational Teacher Education –NTA Level 5)

Muda: Mwaka mmoja Sifa za kujiunga: Stashahada ya Ufundi katika sekta za ufundi, sawa na ‘Ordinary Diploma – NTA Level 6’ inayotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

2 ADA NA GHARAMA NYINGINE ZA MAFUNZO

Ada za mafunzo kwa kozi zote za Cheti kwa sasa ni Shilingi 345,400 (Laki Tatu Arobaini na Tano Elfu na Mia Nne). Gharama za Chakula, Mazoezi kwa Vitendo, Vitabu pamoja na Mchango wa Serikali ya Wanafunzi zimefafanuliwa kwenye kiambatisho (Fee Structure) kinachopatikana katika tovuti ya Chuo - www.mvttc.ac.tz

3 UTARATIBU WA MAOMBI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO

Maombi ya kujiunga na mafunzo yanafanywa kwa kujaza fomu inayopatikana kutoka tovuti ya VETA: www.veta.go.tz au MVTTC: www.mvttc.ac.tz kwa gharama ya Shilingi 10,000 tu. Maelezo ya namna ya kulipia fomu yanapatikana ndani ya fomu.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 Machi, 2021.

Kwa maelekezo zaidi wasiliana na Afisa Udahili kupitia namba za Simu: 0762609788 au 0682888224.

Tangazo hili limetolewa na

Mkuu wa Chuo

Chuo Cha Ualimu wa Ufundi Stadi MorogoroTarehe: 25 February, 2021


0 Comments