Katika somo hili utajifunza namna ya kuandaa kifaa chako na utangulizi wa somo.

MAFUNZO YA PHP SOMO LA KWANZA

Mahitaji ya course:
1.Uwe na kompyuta ama smartphone
2.Uwe na uelewa wa html
3.Uwe mjanga, wa kuweza kutumia simu ama kompyuta yako vyema
4.Ujuwe kusoma na kuandika
5.Kuwa na hamu ya kutaka kujuwa.

Utangulizi:
PHP ni katika lugha za kikompyuta inayotumika kwenye server. Php hutumika katika kutengeneza kurasa za wavuti kama ilivyo html. Php pia inaweza kutumika katika kutengeneza software. Php ni moja katika lugha zinazotumika sana katika blog kama wordpress na katika social media kama facebook. Php ni free kibiashara na hata binafsi.

Php ilianzishwa mwaka 1994 na mmarekani aliyejulikana kwa jina la Rasmus Lerdorf, ikiwa kama home project. Nika katika luga za kikompuata zilizo rahisi kujifunza, hata hivyo syntax yake inaweza kuwa ngumu kuliko javascript na lugha nyingine.

PHP ni nini?
Php ni kifupisho cha maneno Hypertext Preprocessor. Php hutengeneza kurasa za wavuti kama html, pia huweza kutumiwa ndani ya html ama html ikatumiwa ndani ya php. Kwa pamoja tukaweza kuhama kutokakurasa kwenda kurasa ndio maana php ikawa nayo ipo katika hypertext kama ilivyo html. Tofauti ni kuwa php kwanza code hufanyiwa processing kwenye server, kisha ndipo server hutuma matokeo kwenye browser kama html code ama plain text kwa maana hii ndipo tunapata preprocessor kwa maana kwana code zinachakatwa kwenye server kisha matokeo ndipo hutolewa kama html ama plain text kwenye browser.

NINI PHP HUFANYA:
1.Hutengeneza dynamic web page
2.Hutengeneza static webpage
3.Huwengeneza web App

Kwa ufupi php ina uweza kufanya mambo haya:-
1.Inaweza kuedit data kwenye database
2.Kuongeza na kupunguza data kwenye database
3.Kujaza fomu za madodoso
4.Kupokea taarifa kutoka katika madodoso (form)
5.Kufunga na kufunguwa database
6.Kufunguwa na kufunga mafaili
7.Kutengeneza dynamic na static web page
8.Kutengeneza system za web App

PHP inafanyaje kazi?
Kwanza browser inapokutana na code za php, code hizi hutumwa kwenda kwenye server. Server inachakata code za php na kurudisha matokeo kwenye browser kama plain text, na hapo html huchukuwa nafasi yake, hatimaye maudhui yanaonekana kwenye browser kama html.

Server ni nini?
Server ni kompyuta inayohudumia kompyuta nyingine. Zipo kompyuta maalumu zinafanya kazi ya kuhudumia kompyuta nyingine, lakini kompyuta yako mwenyewe pia unaweza kuifanya iwe server na kuhudumia kompyuta nyingine. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia sikuhisi hata simu inaweza kuwa server na kuhudumia kompyuta.

Browseer yako kama chrome, firefox na opera zinaelewa html, javascript, xml, css lakini haziwezi kuelewa php. Hivyo ili code za php uweze kuzirun kwenye browser ni lazima uwe na server ambayo inachakata php na kurudisha majibu kama plain text.

KUIANDAA SIMU NA KOMPYUTA YAKO KUTUMIA PHP
Kama nilivyokueleza kuwa php inahitaji server. Hivyo unatakiwa uwe na App ambazo zitaweza kufanya simu yako iwe localhost server. Fuata hatuwa zifuatazo:-
1.Katika simu yako tengeneza folder liite website
2.Download App hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sylkat.apache kama unatumia simu ama download xamp au wampserver kama unatumia kompyuta.
3.Download App hii kama unatumia simu https://play.google.com/store/apps/details?id=com.rhmsoft.code ama kama unatumia kompyuta unaweza kutumia notepad, ama sublime text, au notepadplus.
4.Funguwa App hiyo hapo juu kama unatumia simu, kisha pest code hizo hapo chini.

print â€Å“hello my php”;
?>
5.Kishha sevu, utaona kialama cha kusevu chini. Utaletewa kuchakuwa folda la kusevu. Hapo chaguwa lile folda uliolitengeneza. Wekajina kisha weka .kisha wepa php. Mfano index.php.

6.Baada ya kusevu chini utaona kibatani cha kuplay. Bofya hicho kurun code zako hapo maneno haya yatatokea â€Å“hello my php”

7.Hapo utakuwa tayari kwa somo.

KWA WATUMIAJI WA KOMPYUTA:
1.Kama umedownload xamp ingia kwenye folda lililoandika htdocs, hapo tengeneza folda lingine liite website.
2.Kwa waliodownload wampserver tafuta folda lililoandikwa www ingia hapo kisha tengeneza folda lingine liite website
3.Funguwa notepad kisha pesti code hizi
print "hello my php";
?>

4.Sevu kwenye folda la website ulilotengeneza hapo juu. Weka jina kisha weka doti kisha weka php. Mfano index.php
5.Funguwa browser yako kisha andika localhost kwenye upau wa link.
6.Utakapofunguka ingia kwenye folder la website kisha bofya faili lako ulilotengeneza kwa code hizo hapo juu. Browser italete matoke kwa text hizi â€Å“hello my php
7.Kama umefika hatuwa hii basi upo tayari kuendelea na somo.

Usikose somo lijalo litakalokuja kuangalua zaidi kuhusu php na kanuni zake za kuandika project.

Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass

Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bodya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp 💧 bofya hapa

0 Comments